skip to main |
skip to sidebar
BIFU LA ALIKIBA NA DIAMOND LAPOTEZA MWELEKEO WA OMMY DIMPOZ
Msanii wa bongo fleva Ommy Dimpoz ni moja kati ya wasanii wanaoathiriwa
na kuwepo kwa ile bifu kati ya Team Diamond na Team Kiba kwa kuwa wote
ni washikaji zake. Ommy amesema kuwa mashabiki wanamweka katika wakati mgumu kwani
akionekana yuko na mmoja wapo... anaonekana snitch kwa wengi na kusema yeye
hajaegemea upande wowote bali ana focus na mambo yake.
“Yanapotokea matatizo kama haya hutakiwi ku choose side,unayaangalia
yapite kwa sababu naamini yataisha,mimi najaribu ku focus kwenye mambo
yangu binafsi.Ukisema uegemee upande huu utazua matatizo mengine bora
niyasome kama shabiki.” alisema Ommy Dimpoz alipoulizwa kwanini urafiki
wake na Diamond umepungua.
0 comments:
Post a Comment