“Siku zote maisha ni kuchagua na kupanga, kama ikitokea nikahitaji kuongeza watoto zaidi ya wawili basi itakuwa... hivyo ila mpango wangu ni wawili tu wananitosha ili mke wangu aendelee kuwa kwenye ubora wake na siyo kumchosha.
“Kwa upande wa mwanamke ninayempenda na kuhitaji awe mke wangu na mama wa watoto wangu ni yule tu mwenye sifa zifuatazo;
Hofu ya Mungu
“Akiwa na hofu ya Mungu, atajiheshimu, atakuwa na upendo, atakuwa na huruma kwangu, watoto na familia nzima kwa ujumla na hii itasaidia kujenga familia iliyo bora mfano wa kuigwa. Pia atajilinda na kujithamini kama mke wa mtu ingawa majaribu anaweza kuyapata kama mwanadamu mwingine ila kwa sababu ya hofu ya Mungu anaweza kuyashinda na kuyaepuka.
Aidha, atakuwa mcha Mungu kwa kwenda kwenye ibada jambo litakaloifanya familia yetu kuishi kwa kufuata taratibu za Mungu.
Mwaminifu
“Hakuna kitu kinachoumiza katika uhusiano wa mapenzi kama uaminifu kwa hiyo sihitaji kuumia, napenda kupata mwanamke ambaye atakuwa ni mwaminifu kwa kila kitu, akiwa mwaminifu ni dhahiri ni mtu ambaye anajitambua.”
‘Smart’ kichwani
“Ukiachana na ishu ya elimu, napenda mwanamke ambaye kichwani mwake ni smart, ambaye tunaweza kukaa na kushauriana na akashauri vitu, mwenye hoja au kama kuna kitu anapinga basi anapinga kwa hoja, hii itasaidia sana katika ushauri wa familia, muziki, biashara na hata maisha yetu kwa ujumla. Namaanisha mtu ambaye tunaweza kukaa na kushauriana kuhusu maendeleo ya familia yetu kwa ujumla ikiwa ni pamoja na wazazi na ndugu zetu.”
Upendo
“Upendo ni kila kitu katika maisha ya mwanadamu, Mungu anatuagiza kuwapenda ndugu, jamaa, marafiki na hata maadui zetu, sihitaji kuwapoteza ndugu, jamaa au mashabiki wangu kwa sababu ya kuwa na mwanamke asiye na upendo. Mtu asipokuwa na upendo atasababisha chuki na mifarakano ndani ya nyumba yetu jambo ambalo sipendi lije kutokea.
“Ukiachana na sifa za mwanamke ninayempenda kwangu kazi ndiyo kila kitu, niliamua kusafiri na kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya remix ya video ya wimbo wangu wa Zigo ambao nimemshirikisha Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuna kitu kilinishangaza baada ya Wazungu kuvujisha picha za wimbo huo ambapo sisi tulitaka tufanye kama sapraizi kwa Watanzania.
“Kingine kilichonishtua ni kusikia wimbo wangu wa Zigo remix umekatazwa kuchezwa mchana mpaka usiku ambapo watoto watakuwa wamelala hii ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawa-siliano Tanzania, (TCRA), nashangaa kwa sababu ninaona baadhi ya video za wasanii wengine zinaendelea kuchezwa lakini sioni kama kuna hatua yoyote inachukuliwa.
0 comments:
Post a Comment