Hii
ni aibu yao! Picha zinazomuonesha staa wa Hip Hop anayetamba na ngoma
ya Shika Adabu Yako, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa katika
pozi la nusu utupu na msanii wa Bongo Fleva, Aisha Nyange ‘Dayna’
zimevuja pasipo wenyewe kujua.
Katika
baadhi ya picha hizo, Nay anaonekana akiwa amemkumbatia Dyna huku
wakiwa hawana nguo za... juu, yaani Nay hana vesti wala tisheti na hata
Dyna akiwa hana nguo yoyote ya kumstiri juu.
Baada
ya kuzidaka picha hizo gazeti hili lilivuta waya na kuwatafuta wahusika
ambapo baada ya kumpata Nay na kumdadisi kama anabanjuka kimalovee na
mwanadada huyo alikuwa na haya ya kusema;
Dah,
hapana bwana, hizo picha hatukupanga zitoke. Kuna ambazo zilipitiliza
si unajua wakati wa kupiga studio zipo ambazo huwa hamzitumii sasa sijui
nani alizivujisha hizo mbaya.”
Baada
ya kumalizana na Nay, Dyna naye alitafutwa ili kuifungukia ishu hii,
ambapo baada ya kupatikana alidai zilikuwa ni picha za kwenye kava la
ngoma yake ya Nitulize aliyomshirikisha Nay lakini alipoulizwa kuhusu
zile zilizovuka maadili, alijibu:
“Aah!
Hilo ni suala binafsi, lakini naomba iishie kufahamika kuwa Nay ni mtu
wangu wa karibu lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi, ilikuwa ishu ya
kazi tu.”
0 comments:
Post a Comment