Kuanzia
wiki iliyopita kwenye mtandao wa Twitter kumeonekana kuwa hapatoshi kwa kuwa
busy sana baada ya Witness a.k.a Kibonge Mwepesi kuanzisha kampeni ya kwenye
mitandao kwa kuzitangaza maliasili zetu zilizopo Tanzania zisipotee.
Akiongea
na XXL ya Clouds FM, Witness amesema, “Kubrand maliasili zetu ni jukumu la kila
mtanzania siyo kwa serikali tu peke yake, nchi nyingine wananchi wake
wanajitahidi kutangaza maliasili zao mpaka...
wanapitiliza mipaka kwa kuiongopea
dunia kwa kusema baadhi ya vitu vyetu vipo nchini kwao.”
Sakata
hili la kutangaza maliasili za Tanzania limekuja juu baada ya kuonekana kipande
cha video ikimuonyesha mdada aliyejulikana kama Rosemary Odinga ambaye ni mtoto
wa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Kenya akisema kuwa Olduvai Gorge ipo nchini
Kenya.
0 comments:
Post a Comment