Pages

Subscribe:

Saturday, March 5, 2016

Q-CHIEF: DIRECTOR MWENYE KUTAKA KUFANIKIWA ATAKUBALI KUKOSOLEWA

Q Chief

Q Chief amesema kauli yake ya kusitisha kufanya kazi na directors wa video wa ndani kwa madai hawana jipya, isichukuliwe kama amemhukumu mtu.

Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Q Chief amedai kauli hiyo ambayo aliitoa hivi karibuni, hakumlenga mtu yoyote, kwani alitaka director anayejiona ana tatizo ajirekebishe. “Unajua neno langu mimi sio hukumu kwa mtu mwingine, lakini watu wengi wanasubiri ufe alafu...
ile kauli yako waitumie, lakini flani aliwai kusema hivi na hivi,” alisema Q Chief.

“Mimi sikuzungumza kwa kumtaja mtu fulani au kumkatisha mtu tamaa, mimi bado kijana na bado nahitaji support, sisi kwenye muziki tunategemeana. Lakini director mwenye uchu wa mafanikio ni director ambae anakubali kukosolewa , ndio maana mimi nakosolewa na ninakubali, na kama sitaki kubadilika basi nisinge chukua maoni, 

Nikajiona mimi bora. Kwa hiyo mimi sikumzungumzia mtu mmoja, ndio maana kaka zake walikaa kimya ambao wamemtangulia, pengine wameona Q Chief ameongea kitu fulani kwa kuhitaji improvement ya kitu fulani, aliye nielewa amelewa,” aliongeza Q Chief.

0 comments:

Post a Comment