Msanii wa siku nyingi wa Bongo Fleva hapa nchini Judith Wambura a.k.a
Lady Jaydee amewaomba watanzania wampende yeye kama yeye na si
kumfuatilia kuhusu mahusiano yake kimapenzi.
Jaydee ameyasema hayo katika kipindi cha E News kinachorushwa na
kituo cha EATV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa baada ya mtangazaji Sam
Misago kumuuliza swali kwamba kuna tetesi kwamba karudiana na mpenzi
wake wa zamani Gadner.
”Watu wengi walinipenda kama nilivyo na hawakunipenda nikiwa na mtu
yoyote, sipendi kuelezea mambo yangu binafsi nawaomba watanzania
wanipende kama mimi kama Jaydee na...
si vinginevyo”-amesema Jaydee.
Msanii huyo ameibuka upya na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Ndi ndi ndi ambapo amesema video yake ataitoa itakapokuwa tayari.
Wednesday, March 23, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment