skip to main |
skip to sidebar
NAY: BAADA YA MWAKA 1 NAWEZA KUWA TAJIRI KULIKO MTU YEYOTE TANZANIA
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego baada ya kudai kuwa utajiri
wake kwa sasa ni zaidi ya bilioni 1, amedai baada ya mwaka mmoja atakuwa
tajiri mkubwa kuliko mtu yoyote Tanzania. Akizungumza katika kipindi cha Weekend Chart cha Clouds TV hivi
karibuni, Nay amesema kwa sasa tayari ameshaingia... kwa miguu miwili
katika biashara ya kilimo.
“Mimi ni mtu ambaye naishi maisha ya ukweli na sijawai kufake, kuanzia
mwezi wa sita nimeshaanza kuwekeza, nafikiri hii inaweza ikawa surprise
kwa mashabiki wangu. Nimeshaanza kuwekeza katika kilimo, mimi
nimeshaanza kununua eka kadhaa pengine panapo majaliwa ikifika mwakani
kuna uwezokano wa kuwa tajiri mkubwa kuliko mtu yoyote,” alisema Nay.
0 comments:
Post a Comment