Habari
mbaya! Majibu ya daktari yamemkatisha tamaa Mtangazaji wa Zouk TV,
Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ baada ya kuambiwa kuwa, kutokana na unywaji
wa pombe kali kupitiliza, maini yake yameanza kuharibika na asipochukua
hatua za haraka hali itazidi kuwa mbaya zaidi.
Kwa
mujibu wa mtu wa karibu wa Penny, hivi karibuni mrembo huyo aliyewahi
kuwa mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alikuwa
hajisikii vizuri na mara nyingi alipokuwa akijaribu... kula, alitapika na
kuishiwa nguvu hivyo akaamua kwenda kupima kwenye Hospitali ya AAR
jijini Dar.
Mpashaji
huyo alidai kwamba baada ya Penny kuchukua vipimo vyote, ilibainika
kwenye maini yake kuna tatizo na chanzo chake ni unywaji wa pombe
kali.“Maskini Penny, sasa hivi hana raha kabisa tangu daktari amwambie
ana matatizo kwenye ini, mara nyingi anakuwa mnyonge na mwenye wasiwasi
sana,” kilisema chanzo hicho.
Baada
ya kupokea taarifa hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Penny ambapo
alizungumza kwa upole kuwa angeomba vitu vingine asiviweke wazi kwenye
vyombo vya habari kwani ni mambo ya kidaktari zaidi.
“Kiukweli sijisikii vizuri na hata kuongea sana naona shida. Unajua vitu vya kidaktari siyo vizuri kuviweka kwenye vyombo vya habari. Kifupi sipo vizuri,” alisema Penny akionekana kutokuwa na furaha.
0 comments:
Post a Comment