Mrembo ambaye amewahi kung’arisha vichupa kadhaa vya mastaa Bongo
maarufu kama Tunda amekuwa akitajwa kutoka kimapenzi na rapa kijana
maarufu kama Young D au Paka Rapper.
Hivi karibuni kuna uvumi ulizuka kuwa wawili hao wameacha baada ya
mrembo huyo kufuta baadhi ya picha alizowahi kupiga na Young Dee huku
kati ya zaidi ya picha 480 zilizopo kwenye ukurasa wake wa Instagram
amebakiza...
picha moja tu ya rapa huyo.
Vilevile katika ukurasa wa Young Dee kati ya picha 125 alizowahi kupiga
na mrembo huyo wa vichupa ameiacha picha moja tu, jambo ambalo limeibua
maswali mengi kwa wapenzi wa burudani wanao wafuatilia mastaa hao.
Kupitia kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio
mrembo huyo wa vichupa amefungukia suala hilo na kueleza kuwa yeye na
Young Dee wapo sawa ingawa kuna baadhi ya maneno yake yaliashiria kuwepo
jambo analolificha.
Alipoulizwa kama yeye na Young Dee ni wapenzi alijibu.”ndiyo Mimi na
Young Dee tulikuwa wapenzi”, huku kitendo hicho cha mastaa hao kufuta
picha limekuwa ni jambo ambalo linawatokea mastaa wengi pindi
kunapotokea tofauti kati yao.
Saturday, March 5, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment