Harmonize: Nafanya mpango kuitoa familia yangu kijijini kuileta Dar
Harmonize anang’ara kwa sasa lakini safari yake hadi kufika hapo alipo
leo imekuwa ngumu na yenye misukosuko mingi. Ni msanii aliyetoka kwenye
maisha duni katika kijiji chao kilichopo wilayani...
Tandahimba, Mtwara
kwenye familia kubwa yenye wake wengi wa baba yake ambaye ni sheikh.
Kwa mama yake, walizaliwa watoto watatu huku yeye akiwa mtoto wa pili kuzaliwa.
Baba yake ana wake wengine watatu na watoto wengine takriban wanane
lakini aliachana na mama yake akiwa bado mtoto hivyo amekulia kwenye
familia yenye mama tu. “Mimi nimezaliwa bush kweli, hata umeme hatuujui.
Mimi nimekuja town mwaka 2009 tu,” anasema. Hiyo ni baada ya kushindwa
kuendelea na sekondari baada kuishia kidato cha tatu kutokana na baba
yake kupendelea zaidi mwanae asome elimu ya akhera (elimu ya dini ya
kiislamu)
Dar alifikia kwa dada yake ambako baada ya muda ajikuta akipishana na
shemeji yake na kuamua kuanza kuishi mwenyewe kwa kufanya kila kibarua
kilichojitokeza mbele yake. Kuna wakati hadi alikuwa akilala kwenye
stendi ya basi ya mikoani iliyopo Temeke.
Wakati huu ambao maisha yamebadilika baada ya kusaini na WCB, Harmonize
hajaisahau familia yake na ana mipango mikubwa. “Ninafanya mpango
familia yangu nije niishi nayo vizuri hapa kwasababu kijijini kwetu kuna
mazingira magumu sana sidhani kama mtoto mwenye akili timamu unaweza
ukafurahia aishi maisha ya tabu wakati wewe unaishi maisha mazuri,”
anasema. “Nilikuwa nafanya mpango panapo majaaliwa nilikuwa naongea na
management yangu ili kuwa comfortable zaidi basi ikiwezekana hata
familia yangu isogee hapa.” #Regrann
Thursday, March 24, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment