Pages

Subscribe:

Saturday, June 4, 2016

ALAMA KATIKA LEBO ZA NGUO NA MAANA YAKE

Katika Kila nguo huwa na lebo kwa ndani chini kidogo ya kola au pembezoni lebo   ambayo huashiria maelezo ya kuitunza nguo hiyo ila wengi wetu huwa hatujui maana ya alama hizo, sio nguo zote huwa na maelezo ya alama nguo zingine huwa na maelezo tu japokuwa huandikwa kwa...
lugha  kingereza au nguo zingine utakuta lugha tofauti inategemea imetengenezwa nchi gani. Japokuwa nyingi hutumia lugha ya kingereza.
alama 1.
Utunzaji wa nguo unaanzia kwenye Kufua, Kuipiga pasi na kuianika, lebo hizo zitakueleza unahitaji aina gani ya maji kufua nguo hiyo kama ni maji ya baridi au uvuguvugu.  Unahitaji mashine au kufua kwa mkono, Upigaji wa pasi kama ni moto mkubwa, wastani au mdogo kabisa  na kuianika kama ni juani, kuianika kwenye kamba au kuitandika sehemu tambarare. Kila nguo iko na masharti yake.
alama 2
Je? Umeshawaza hawa madobi wa mitaani wanajua taratibu hizi za matunzo ya nguo au tunatumia mazoea kufua nguo zetu. Usilalamike nguo yako inapauka unajua taratibu za kuianika nguo hiyo?  Mara nyingi nguo inayotoa Rangi inatakiwa kuanikwa sehemu ambayo  haina jua ili kuzuia mpauko huo. Kwani sio jua pekee hukausha nguo hata upepo. Nguo za rangi nyeusi zinashauriwa kuanikwa sehemu ambayo haina jua sana au hakuna jua kabisa.
Aina ya maelezo hupatikana kwenye lebo za nguo .
  1. Dry Clean Only –  Ufue kwa mashine za kufulia tu
  2. Do not Dry Clean –  Usifue kwa Mashine za Kufulia
  3. Do Not Bleach – Usitumie Dawa za  kutoa Madoa
  4. Do not Iron – Usipige pasi
  5. Low Iron – Piga pasi kwa Moto mdogo
  6. Do not Wring – Usikamue nguo hiyo
  7. Dry in Shade – Anika kwenye kivuli (hii kwa nguo ambazo hupauka zikianikwa juani)
  8. Tumble dry –  Unaweza tumia mashine ya mvuke kukausha nguo hiyo
  9. Hand Wash – Fua kwa Mkono
  10. Mashine wash Normal – Unaweza kutumia mashine ya kufulia

0 comments:

Post a Comment