Mkali
wa muziki na CEO wa label ya WCB, Diamond Platnumz amesema label yake mpaka
sasa tayari imeajiri watu 42. Muimbaji
huyo ambaye pia anamiliki, studio ya picha pamoja na studio ya muziki ‘Wasafi
Record’, aliwaambia waandishi wa habari hivi karibuni kuwa kila anachokipata
anagawana na team yake “Tunashukuru
mungu kile tunachokipata tunagawana na wengine, mpaka sasa tayari WCB imeajiri
watu 42, hii ni hatua kubwa sana katika tasnia ya muziki wetu,” alisema
Diamond.
Katika
hatua nyingine, Diamond amesema ni swala la kiungwana kulipa kodi katika kile
anachopita. “Unajua
katika kila penye biashara ni lazima na ni haki kulipa kodi ili pato la taifa
liingie, namna ya...
mapato maana yake nini, serikali inatambua kazi na inailinda.
So serikali ipo na inafanya hivyo, lakini labda kuna nyanja nyingine hawazioni,
kwa hiyo sisi kama tunataka kazi zetu zichangie pato la serikali, lazima tuwe
mstari wa mbele katika kuonyesha nyanja zote za mapato, kwamba tunafanya hichi
na hichi, ridhiki zetu zinatokea hapa na hapa, mishahara yetu tunagawa hivi na
hivi, na kama serikali inavyoagiza katika kiasi hichi tunatakiwa kutoa kiasi
hichi kwa ajili ya serikali. Kwa hiyo tusilalamike tu serikali haifanyi kazi
wakati sisi tunaweza kuwa wa kwanza kuirahisishia serikali kutekeleza majukumu
yake,” alisema Diamond.
0 comments:
Post a Comment