Pages

Subscribe:

Thursday, August 3, 2017

MWIGULU NCHEMBA: CHUKUENI MAGARI WAKIJA KULIPA FAINI WAKAMATENI



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ameagiza Askari wa Uhamiaji kuyachukua magari na boti zinazotumika kusafirishia wa hamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume na sheria na kwa wale ambao watakuja kuwalipia faini nao wachukuliwe wajumiishwe katika kutenda kosa hilo.

Mwigulu aliyasema hayo,wakati alipokwenda kukagua...
maendeleo ya ujenzi wa ofisi za mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) na ofisi mpya ya uhamiaji ya mkoa wa Pwani ambazo zote zipo wilayani Kibaha.

“Haiwezekani mtu aingie nchini kwa makusudi bila kibali halafu inapotakiwa kulipa faini kutokana na kosa hilo atokee mtu kuwalipia faini kwa haraka jambo linalosababisha vitendo hivyo kuenea kwa kasi”alisema Mwigulu.

Hata hivyo Waziri Mwigulu alieleza kwamba ni lazima iangaliwe jamii inapaswa kujiepusha na kushirikiana na kundi hilo ili kupunguza wimbi kubwa la wahamiaji haramu nchini.
“Mkiwakamata pia na magari myataifishe siku hiyo hiyo na kuyapeleka magereza ili yakabebe mawe,na hata mkiwakamata kwenye boti taifisheni hizo boti hakuna kuweka viporo,” alisema Mwigulu.

Kwa upande wake Afisa Uhamiaji Mkoani Pwani ,Plasida Mazengo alisema ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vitendea kazi hali inayosababisha kufanyakazi kwenye mazingira magumu.

0 comments:

Post a Comment