Muigizaji wa filamu na Mfanyabiashara, Jacquline Wolper amefunguka na kusema iwapo mpenzi wake wa sasa (Brown) akimtenda na kumuumiza kama waliopita ataamini kuwa hakuna wa kumwamini kwenye mapenzi na kwamba wanaume wote wana matendo ya kufanana.
Akizungumza na Mwandishi, Wolper
ambaye miezi michache alitangaza kuachana na aliyekuwa mpenzi wake
(Msanii wa muziki) na kisha...
kuweka wazi mahusiano yake na Mwanamitindo
Brown amesema kutokana na kijana huyo pamoja na familia yake kuwa na
imani ya dini anaamini hataweza kumuumiza ingawa binadamu wana
mapungufu.
"Siamini kama BFF anaweza
kunifanyia vitendo vibaya kama nilivyowahi kufanyiwa. Namuamini sana
kutokana na kuwa na hofu ya Mungu lakini bado sisi ni binadamu.
Anaweza
kunikosea kawaida au mimi nikamkosea kwa sababu sisi ni binadamu hiyo
haitafanya nimchyukie lakini akifika huku pa kunifanya niumie kama
nilikotoka nitaamini kuwa hakuna wa kumuamini," Wolper.
Wolper amesema kuwa, Brown ni aina ya mwanaume ambaye alikuwa akimuhitaji katika maisha yake na hatimaye Mungu kasikia kilio chake.
0 comments:
Post a Comment