Mkali wa 'Seduce Me' Ally Salehe Kiba, amefunguka na kusema katu
hataweza kuishi maisha ya kuigiza umaarufu kwani anaamini watu ndiyo
waliompokea kipindi akiwa hana kitu hivyo kujikweza ni kuwatengenezea
watu hao hila mioyoni mwao.
Kiba
alifunguka hayo wakati akitoa ushauri kwa wasanii wachanga kwa
kuwaambia kwamba hakuna kitu kibaya kama kuishi maisha ya kuigiza
umaarufu kwani yanakuwa...
siyo maisha yao halisi.
"Watu
wanashindwa kujua kuwa umaarufu wamepatiwa na watu ambao ni mashabiki
zetu sisi. Sasa kuwa na pesa haimaanishi kuwa uishi kwa kuwakomesha
waliokuweka hapo, usiiishi kwa kuwatengenezea watu hila mioyoni mwao. Kwanz hakuna
mtu mwenye pesa. Pesa zote tunazotamba nazo ni za serikali hivyo mtu
anayejifanya kwamba anapesa azifungie ndani aone jinsi ambavyo maisha
yatakuwa. Hata masuala ya kuvimba ni ya kuacha kwani najua tukipata
majanga tutaungana tu."
Alikiba aliongeza kuwa "Mimi
nikisema niishi kistaa ukweli sijui itakuaje, lakini kwa vile naamini
mimi ni Super Star hivyo siwezi ku-act maisha kwa vile naamini yale siyo
maisha yangu, ingawa wapo watu wengi ambao wanaigiza maisha hayo.
Naamini kuwa kuna watu wanafanya kufurahisha mioyo yao. Lakini kama ni
umaarufu Mzee Majuto mwenyewe ni Star lakini anaishi maisha ya kawaida
sana, maisha ya umaarufu siyo ya kwetu tujaribu kuishi maisha yetu ya
kitanzania.
Akiwaasa wasanii wachanga Kiba amewataka
wasanii hao wajifunze kupitia wakongwe wa zamani kwa jinsi ambavyo
walikuwa wakiishi kwa upendo ikiwa ni pamoja na kusapotiana kwa
kuonyeshana upendo na kushikana mikono.
0 comments:
Post a Comment