Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Sajna amesema bosi wake huyo ambaye pia ni producer wa studio za Tetemesha, alimuacha akiwa...
katika kipindi kigumu zaidi bila mawasiliano, ingawa hawezi kumlaumu moja kwa moja, kwani naye alikuwa anatafuta.
“Sikuondoka kwa Kid Bwoy kwa ugomvi ingawa bosi aliniacha vibaya, wakati amekuja kutafuta kazi huku, na mimi nilikuwa namuuguza mama, na muziki ulikuwa ndio kazi yangu, mara ya kwanza niliongea nae kid Bwoy akanitumia pesa kidogo, tangu anitumie hiyo pesa hakunitumia tena mpaka mama alifariki, lakini hakuja kwenye msiba, sasa hata kama kuna mazingira magumu hata kwa ubinadam lazima uangalie”, alisema Sajna.
Sajna aliendelea kusema kuwa ingawa wana muda mrefu hajawasiliana na bosi wake huyo wa awali, lakini anatamani kufanya naye kazi tena kwenye studio zake za Tetemesha, na iwapo atapata kazi akiridhia anaweza akenda kurekodi kwake.
0 comments:
Post a Comment