Msanii Shilole ameweka wazi kile ambacho watu wengi walikuwa hawafahamu
kuhusu watoto wake, na kusema kwamba mambo yake ya mitandaoni
hayawaathiri na badala yake wako vizuri darasani huku mmoja wao akiwa na
ndoto kubwa ya kugundua dawa ya UKIMWI
Akizungumza na mwandishi wa habari Shilole amesema pamoja na kwamba yeye hajapata bahati ya kusoma, lakini watoto wake wako makini na shule huku...
akiwaonya na kuwasisitiza kuwa makini, kwani iwapo watafanya vibaya watakuwa wanamuangusha kutokana na anayoyapitia kwa ajili yao, hivyo wanazingatia ipasavyo kauli ya mama yao na kutojihusisha na mambo ya mahusiano yake.
"Wanangu hawana shobo na haya mambo, wanataka niwe na furaha, ndio maana hujaona watoto wangu wameniangusha kwenye masomo kwa vitu vya kusikia kwenye mitandao, ndio kwanza wanaongoza namba moja, namba mbili, nawaambia mkifanya blanda mnaniangusha mimi, mkifanya tukio mjue mnanizika, kwa hiyo watoto wangu wapo makini na masomo kuliko kitu chochote, huyu mmoja anasoma aje kuwa dokta ili aje agundue dawa ya UKIMWI, kwa nini uliletwa, na anafanya vizuri darasani", alisema Shilole.
Shilole ambaye ana watoto wawili wote wakiwa wa kike, anasema anajisikia faraja kuona watoto wake wanapa fursa ya kufanya yale ambayo yeye hakufanikiwa kuyafanya, ikiwemo kupata elimu bora ambayo anaamini itakuja kuwasaidia baadae kwenye maisha yao.

0 comments:
Post a Comment