Sasa leo September 3, 2017 nimekusogezea hii stori ambapo unaambiwa...
Wanasayansi wameelezea kuhusu kwa nini mtu hukosa usingizi au kutolala vizuri akiwa ugenini wakisema husababishwa na ubongo.
Mtu anapolala ugenini au mahala asipopazoea nusu ya ubongo wake ndiyo hulala lakini nusu nyingine inakuwa ‘active’ na hii ni kutokana na mabadiliko ya mazingira.
Unaambiwa jambo hili hupelekea mtu kuchelewa kupata usingizi na huwahi kuamka pengine isivyo kawaida na wakati mwingine awapo katikati ya usingizi huweza kushtuka anaposikia milio ya vitu kama ndege, mtu anatembea na vingine vingi.
0 comments:
Post a Comment