Muimbaji nguli wa Kenya, Nameless
amewazungumzia Diamond na Alikiba na tofauti walizonazo kimuziki. Akijibu swali la mtangazaji wa kipindi
cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe, Divine Kweka kuhusu nani mkali kati ya
wasanii hao wawili, staa huyo ambaye ni mume wa staa mwingine wa Kenya, Wahu,
alisema wote ni wakali kwa sababu tofauti.
“Kwa kweli naona kila mmoja ni mkali
for different reasons,” alisema Nameless.“Namheshimu Kiba kwasababu naweza
kusema bado anafanya mambo makubwa na amekuwa...
kwenye industry kwa muda mrefu
kwahiyo hapo ndipo nampatia heshima.”
“Halafu nikiangalia Diamond nampatia
heshima kwasababu kwakweli amefanya mambo mapya makubwa zaidi lakini yeye
naweza kusema ni younger new artist kuliko Alikiba kwahivyo kwake nampa heshima
kwasababu ya kufanya mambo mapya makubwa zaidi na kwa Alikiba nampatia heshima
kwasababu anaendelea kufanya mambo mazuri na makubwa kwa muda mrefu, amekuwa
kwenye game kwa muda mrefu sana,” alisisitiza.
Nameless pia amezungumzia muziki wa
Afrika kwa jumla na familia. Msikilize zaidi Nameless akiongea hapo chini.
0 comments:
Post a Comment