Mwanariadha raia wa Kenya David Rudisha amedhihirisha ubora wake baada ya kushinda mbio za mita 800 mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil usiku wa kuamkia leo. Mwanariadha huyo mwenye miaka 27 ameonesha uzoefu wake katika mbio ambapo baada ya kuwa nyuma alianza...
kuwapita wenzake katika mzunguko wa mwisho na hata Mkenya mwenzake Alfred Kipketer na kukamilisha mbio hizo kwa dakika moja na sekunde 42.15
Ushindi wa Rudisha umemfanya kuwa mwanariadha wa kwanza kushinda mbio hizo katika mashindano mawili mfululizo tangu 1964. Rudisha alisema, "kukimbia kwa muda wa 1:42, ni kitu cha ajabu, sikuwa na mashaka kabla, najisikia vizuri sana katika mwili wangu".
"Ni jambo kubwa sana kushinda shindano kubwa kama hili, ni dhahabu yangu ya pili, ni kubwa sana, ni wakati mkubwa sana katika kazi yangu" - aliongeza Rudisha.
Naye Taoufik Makhloufi raia wa Algeria alishika nafasi ya pili na kujinyakulia medali ya 'Silver' kwa kikimbia kwa dakika moja sekunde 42.61.
0 comments:
Post a Comment