Wasanii wanne wa kundi la vichekesho la Orijino Komedi akiwamo meneja
wao wamekamatwa na kuhojiwa na jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam kwa kosa la kuwa na sare za polisi.
Juzi, jeshi hilo lilitoa onyo kwa mtu ama kikundi chochote kuacha
kutumia mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na majeshi ya ulinzi na
usalama nchini na kwamba... atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai, sura ya 16 na marejeo
yake ya mwaka 2002, kifungu cha 178 (1) na (2) kinachozungumzia makosa
dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama, kinabainisha kuwa ni kosa
kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na
usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi
hayo bila kibali kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo, Hezron Gyimbi alisema wasanii hao
walikamatwa juzi saa 10 jioni baada ya kusambaa kwa video kwenye
mitandao ya kijamii wakiwa wamevalia sare hizo kwenye sherehe ya harusi
ya Emmanuel Mgaya maarufu ‘Masanja’.
Gyimbi aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Lucas Lazaro (Joti), Alex
John (McRegan) na Isaya Gidion (Wakuvanga) na Sekioni David (Seki)
ambaye ni meneja wao.
Alisema sare walizokutwa nazo watuhumiwa hao ni za kazi za kawaida za
jeshi la polisi hilo ikiwamo kofia, filimbi, shati, suruali, cheo na
mkanda.
“Tunaendelea kuwachunguza zaidi kama wana vitu vingine vya jeshi la
polisi na tunataka kujua kuwa sare hizi wamepa- ta kibali kwa nani na
uhalali wa kuwa nazo,” alisema Gyimbi.
Alisema jeshi hilo linaendelea kumtafuta Masanja ili kujibu tuhuma
zinazomkabili. Kaimu kamanda huyo alisema watuhumiwa hao walihojiwa
katika Kituo Kikuu cha Polisi kuanzia juzi saa 10 jioni hadi jana jioni
huku na dhamana zao zilikuwa wazi.
Thursday, August 18, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment