Pages

Subscribe:

Wednesday, August 31, 2016

TCRA: MIAKA 20 JELA KWA ATAKAYE POST PICHA ZA UTUPU (UCHI) MTANDAONI

Kwa mara nyingine tena, mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA imewakumbusha watanzania kutozichezea sharubu za sheria ya makosa ya mtandaoni, lasivyo wataishia pabaya.

“Ni vyema wananchi wakatambua kwamba uchochezi kwenye mitandao kwa kusambaza ujumbe wenye viashiria vya uvunjifu wa amani au kuweka picha zisizofaa kwenye mitandao sheria ipo wazi na watu watajikuta wanaishia pabaya, hivyo... ni vyema kuchukua tahadhari mapema,” alisema Mhandisi wa Mawasiliano wa Victoria Rulakara wakati akizungumza kwenye kipindi cha Hotmix cha EATV.

Wakati huo huo, mamlaka hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ikiwa ni pamoja na kuwaonya watu wanaonzisha blog zenye majina ya uongo kutukana watu wengine.

Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ilipitishwa mwaka jana na rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

0 comments:

Post a Comment