Msanii mkongwe katika muziki wa bongo fleva, Dully Skyes amefunguka na kusema kuwa watu wengi wanamfananisha mavazi yeye na msanii kutoka Marekani Kanye West ndiyo maana hata yeye amekuwa akitokelezea kama msanii huyo.
Akiongea
na chombo kimoja cha habaari Dully Skyes alisema kutokana na watu kumfananisha na Kanye West
kwenye mavazi ndiyo maana hata kwenye video ya wimbo wake mpya wa
'Inde' amevaa...
nguo zenye 'Logo' ya Kanye West 'Yeezus'.
"Mimi watu wengi hunifananisha mavazi yangu na Kanye West, ndiyo maana napenda kuvaa kama Kanye West ndiyo maana nikaamua kuvaa hii 'Yeezus' ingawa yeye anamaanisha 'Jesus' lakini mimi nimevaa kwa sababu ya Kanye West ila sijavaa kwa sababu ya 'Jesus'" alisema Dully Skyes
Mbali na hilo Dully Skyes alisema kuwa yeye alifeli shule ila hawezi kufeli kufanya muziki kwani amezaliwa kwenye familia ya muziki hivyo anajua muziki.

0 comments:
Post a Comment