Pages

Subscribe:

Wednesday, August 10, 2016

BEN POL: SINA CHUKI NA WASANII BALI TUNASHINDANA TU


Mkali wa muziki wa Rn'B nchini Tanzania, Ben Pol amefunguka kuwa hana kinyongo na wasanii wenzake ambao wanafanya muziki unao endana bali wanashindana na ndiyo maana inaathiri kazi wanazo fanya pamoja. Ben Pol ameeleza hayo mbele ya camera ya eNewz baada ya kuulizwa kuhusiana na project aliyowahi kuifanya na Jux katika wimbo wa Mwambie na kisha wimbo huo...
kufa bila kufika mbali wakati umeimbwa na wasanii wakubwa.

Ben Pol ameeleza "Unaweza kupanga tufanye joint ya pamoja, lakini unakuta ukirudi studio una kazi yako binafsi na unataka kuisimamia kazi yako binafsi na kushindwa kufanya ya pamoja, Hilo linasababisha kuweka mkazo kwenye kazi binafsi na kusahau ya pamoja"

Pia Ben Pola amesema alishafanya kazi na Baraka De Prince lakini ikashindwa kufanikiwa kwa kuwa wanafanya muziki unao endana na wote wapo kwenye ushindani. Wimbo wa mwambie ambao ulifanya vizuri Ben Pol anasema ulishalipiwa hela ya video lakini haikufanikiwa.

Kwasasa Ben Pol amefanya kazi na Sterio katika wimbo uitwao shilingi, na amekanusha kuwa wimbo huo utakufa kama vyimbo zilizopita kutokana na kwamba yeye na Sterio hawafanyi muziki ambao unafanana hivyo ni rahisi kuupa promo muziki wao.

0 comments:

Post a Comment