Msanii bingwa wa masauti Christian Bella, amezungumzia 'conditions' ambazo anataka awe nazo msanii anayemsimamia, ili waweze kwenda sawa na kufika kimuziki. Akizungumza Christian Bella amesema msanii anayemsimamia anataka awe na uwezo mzuri, ili akitoa kazi ifanikiwe, na isipofanikiwa hataweza kukaa na mtu ambaye hawezi kazi na asiye na nyota.
"Mi sipendi msanii wangu anayeimba na mimi akafanye collabo, akaimbe ngoma tatu nne zinafeli, inaonekana kama mimi nahifadhi mtu ambaye hana nyota, kwa sababu msanii ambaye niko naye anatakiwa...
akitoa ngoma yake ya kwanza akitambulisha atoboe, ikifeli nitamwambia kwanza mara ya kwanza bwana ee, hii sio nzuri, naendelea tena , inaonekana kama haniheshimu, mara ya pili ya tatu nitampa condition ya mwisho, isipohit sikutaki kwa sababu nataka nione kama kweli una nyota, siwezi kuhifadhi mtu ambaye hana nyota", alisema Chrisrian Bella.
Christian bella aliendelea kusema kwamba iwapo msanii huyo atafanya poa basi hata yeye mwenyewe ataweka nguvu zake kumsapoti, ili mradi awe mpiganaji kweli.
"Na ikienda kwenye media naweka nguvu zangu, mimi ndiyo naanza kumtambulisha, tukienda kwenye show namwambia perfom ngoma yako mpya, we si umetoa ngoma, nenda kaiperfom, anaogopa kuperfom sasa wewe msanii gani umetoa ngoma unaogopa kuperfom, nakuhifadhi kwa nini, wewe sio soldier, nahitaji watu ambao wanaweza ku 'fight' ", Alisema Christian Bella
0 comments:
Post a Comment