Monday, October 3, 2016
BABY J AELEZA SABABU YA MUZIKI WA ZANZIBAR KUTO HIT
Msanii wa muziki kutoka visiwani Zanzibar, Baby J ambaye kwa sasa upo chini ya usimamizi wa Mkubwa Fella amefunguka na kueleza kwanini kuna wasanii wachache wa muziki wa Zanzibar ambao wanafanya vizuri Tanzania Bara. Akiongea wiki hii, Baby J amesema mpaka sasa bado hawajajua sababu ni nini lakini wameliona hilo tatizo na wameanza kuchukua hatua.
“Kwanza muziki wa Zanzibar upo tofauti na huku ndio maana kila siku ameshazoeleka kusikika Baby J,” alisema Baby J. “Lakini wanamuziki wapo Zanzibar ambao wanafanya...
vizuri na wapo ambao wana uwezo mkubwa tu lakini kila siku tunasikika wasanii wachache kwa sababu ya ugumu kidogo wa game kwa upande wetu,”
“Ugumu huu unatokana na kutokuwa na support yakutosha, lakini mimi nashindwa kuelewa ni nini tatizo, muziki wa bongofleva wa Zanzibar unapendwa sana huku, lakini tumeanza kujichanganya zaidi na wasanii wa huku bara ili kutafuta mabadiliko,” aliongeza Baby J.
Wasanii wa Zanzibar wiki iliyopita waliungana na wasanii wa bara na kucheza mechi ya hisani dhidi ya wasanii wa filamu kuchangia waathirika wa tetemeko Bukoba.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment