Mwanzilishi wa kundi la LFLG rapa Billnas ameunga mkono tuhuma za Nuh
Mziwanda kwa kumshukia meneja wao Petit Man juu ya uongozi mbaya na
upigaji wa hela kupitia mgongo wao. Billnas akipiga story za eNewz na kusema kuwa matatizo ni kweli
yametokea lakini akamshauri Nuh Mziwanda ni vyema kwa sasa wakatafuta
namna ya kumaliza mzozo huo.
"Petit ni mmoja kati ya watu wa LFLG, So kama mmoja wetu ana matatizo
then wengine wanaweza kutumika kusuluhisha, au vinginevyo anaweza
kupunguzwa ili...
wengine waendelee vizuri na kazi" aliongeza Billnas.
Hapo awali mzozo kati ya Petit Man na wasanii anaowasimamia yaani Nuh
Mziwanda na Billnas ulianza kusikika baada ya Nuh Mziwanda kujitoa chini
ya usimamizi wa Petii Man kwa madai kuwa ni "mpigaji" na kwamba hutumia
majina yao vibaya kupata pesa na pia si meneja anayewajali wasanii
wake.
Saturday, October 1, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment