Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye kwa sasa anatamba
vizuri na wimbo wake ‘Salome’ amefunguka na kusema kuwa wimbo huo
uliwavuruga wasanii wengi wakubwa duniani kabla hajatoka hata baada ya
kutoka.
Diamond Ploatnumz alisema hayo kwenye Friday Night Live (FNL) na
kudai kuwa wimbo huo yeye mwenyewe anashindwa kuelewa una nini kutokana
na jinsi ambavyo umeweza...
kupokelewa vizuri na kupendwa na watu wengi
sana duniani.
“Kiukweli kabisa hata wakati napata wazo kusema nifanye wimbo wa
‘Salome’ nilikuwa nasema ni wimbo fulani mzuri kiasi kwamba hata mtu
asipoelewa lugha lakini anaweza kuipenda, nikumbuka hata wakati Mama
yule Said Karoli alipoimba wimbo ule na ulipokuwa unavuma tulikuwa
hatuelewi anazungumza nini lakini tuliipenda na ilikuwa nzuri na ilivuma
sana, kwa hiyo nikasema kwa sasa hivi soko lilivyokuwa na nikiwatizama
Watanzania nikichukua wimbo ule nikatia vitu vyangu fulani hivi itakuwa
kali zaidi.
Saizi wimbo huu Afrika na sehemu ambazo wanatutizama imekuwa kubwa
nafikiri watakuwa wameipenda sana hata ukiangalia ‘Comments’ zao kwenye
video ile ‘Youtube’ unaona kuwa wameipenda.
Kabla ya wimbo kutoka Wizkid alikuwa Tanzania wakati nipo naye
nilimpa ule wimbo aisee ulimvuruga sana, nilipata bahati ya kuwa na
Mheshimu Rais Mstaafu Jakaya Kikwete naye aliupenda sana, hata baada ya
wimbo kutoka wasanii wakubwa kama wakina Teckno, Flavour walinitumia
ujumbe mfupi kuonyesha kupenda nakumbuka hata Neyo naye aliniambia ‘I
like the song’” alisema Diamond Platnumz.
Sunday, October 9, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment