skip to main |
skip to sidebar
WEMA ACHARUKIA WANAO MSEMA ZARI NA AUNT EZEKIEL
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, amefunguka kuwa anachukizwa na watu
wanaomtolea matusi muigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel, baada ya
kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mzazi mwenza wa Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Akizungumza na Za Motomoto News, Wema alisema unatakiwa ufike wakati
watu waelewe na waongozwe kwa akili zao za kuzaliwa kwa sababu hakuna
kitu kibaya ambacho amekifanya Aunt, kwa kuwa... staa mwenzake huyo kwa
sasa ni mmoja wa familia hiyo.
“Jamani hebu naomba kwanza wamuache Aunt, hana kosa lolote, hata kama
ningekuwa mimi hapa nisingeweza kuacha kwenda kwa sababu tayari ni
familia na hawezi kumuacha mumewe aende peke yake maana vitu vingine ni
vya kujiongeza tu, nachukizwa sana na jinsi wanavyomrushia maneno ya
kashfa,” alisema Wema.
0 comments:
Post a Comment