Msanii wa muziki wa bongo fleva Najma ambaye ni mchumba wa Baraka The
Prince amefunguka na kusema hakutegemea kuwa katika mahusiano na Baraka
The Prince lakini alijikuta tu ameingia kwenye mahusiano na msanii
huyo.
Najma alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema awali hakutegemea kama angekuwa katika mahusiano na msanii huyo.
"Kiukweli kabisa mimi wala sikutegemea kuwa na Baraka The Prince sema imetokea, nashukuru Mungu tunapendana saizi yeye ndiye...
ananichagulia hata nguo za kuvaa akiona sijapendeza ananiambia hata kama kitu mimi nimependa yeye asipopenda nabadili, kwa hiyo tunapenda sana" alisema Najma
Kwa upande wake Baraka The Prince alisema kuwa ni mapenzi ni moyo wa
mtu wala si kabila au ushamba ni vile watu wawili mnavyopenda na
kukubaliana na ndiyo kitu kilichotokea kati yao.
Najma alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema awali hakutegemea kama angekuwa katika mahusiano na msanii huyo.
"Kiukweli kabisa mimi wala sikutegemea kuwa na Baraka The Prince sema imetokea, nashukuru Mungu tunapendana saizi yeye ndiye...
ananichagulia hata nguo za kuvaa akiona sijapendeza ananiambia hata kama kitu mimi nimependa yeye asipopenda nabadili, kwa hiyo tunapenda sana" alisema Najma
"Unajua mimi ni Msukuma na
natoka Mwanza lakini nikwambie kitu mapenzi siyo kabila wala sehemu
unayotoka, maana unaweza kuwa unatoka mkoani lakini ukawa mjanja na wapo
wengine wanatoka mjini lakini washamba, kwa hiyo mimi na Naj
tunapendana na tumekubaliana na ndiyo maana unaona tuko pamoja mpaka
sasa" alisema Baraka The Prince.
0 comments:
Post a Comment