Pages

Subscribe:

Wednesday, July 19, 2017

HII NDIYO SABABU YA LINEX KUTO MSAHAU CHID BENZ

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Linex Sunday Mjeda ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Got Me' amefunguka na kusema kitu ambacho alikifanya Chid Benz katika maisha yake ya muziki hawezi kuja kumsahau. 

Linex amesema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio na kudai kuwa Chid Benz ndiye alikuwa chanzo cha yeye kuachana na...
kufanya muziki wa rap na kujikita katika muziki wa kuimba mpaka amekuja kufanikiwa. 

"Mimi sijawahi kuacha kuwa shabiki wa Chid Benz kama mlikuwa hamjui Chid Benz amekuwa chanzo cha muziki wangu, nakumbuka wakati wa nyuma nilikuwa nafanya muziki wa rap nilimfuata Chid Benz ili nifanye naye collabo, nilipofika Ilala alinipokea vizuri sana na kunikaribisha ndani kwake, akaniuliza mdogo wangu unataka kinywaji gani mimi nikafunga nikaomba maji ya kunywa baada ya hapo nilimpa kazi yangu akaisikiliza kisha akaniambia mdogo wangu siwezi kufanya kazi yako sababu ipo kisela sana," amesema Linex 

Linex aliendelea kuelezea namna ambavyo Chid Benz alimfanya kuachana na huo muziki wa kisela na kuanza kujitafuta na kufanikiwa katika muziki wa kuimba.

"Baada ya hapo Chid Benz alinisikilizisha nyimbo kali kibao ambazo amefanya na wasanii wengine ambazo zilikuwa hazijatoka bado, kisha akaniambia kuwa napaswa kufanya kazi kama hizo, baada ya hapo niliondoka na kuachana kabisa na kuimba muziki ule, nikaacha hata kurekodi nikatafuta band na kwenda kujifunza muziki wa kuimba na huko ndipo nilijipata Linex na kuanza kufanya muziki wangu ambao ulinitambulisha vizuri, kwa hiyo utagundua haya yote ni matokeo ya Chid Benz". Alisisitiza Linex Mjeda

Chid Benz wiki kadhaa alipokuja kwenye kipindi cha Planet Bongo alisema kuwa katika muziki huu wa bongo fleva amekuwa msaada mkubwa kwa wasanii wengi sana ambao alikuwa akishirikiana nao kwenye kazi zao na kuwafanikisha, huku akisema wakati ana nafasi kwenye muziki alikuwa anaishi vizuri na watu wengi ndiyo maana wapo baadhi ya wasanii wanaona wana kila sababu ya kulipa fadhila kwake kwa kile alichokuwa akikifanya kipindi ambacho yupo kwenye nafasi nzuri.

0 comments:

Post a Comment