Msanii wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma ya Utamu, Lulu Diva amedai
katika vigezo ambavyo anavyoangalia wakati wa kuingia kwenye mahusiano
ni pamoja na mwanaume mwenye shahuku ya mafanikio lakini pia atakayeweza
kumvulia na kuwa msikivu.
Diva
huyo anayekuja kwa kasi kwenye 'game' ya bongo ameeleza kuwa licha ya
kuhitaji mwanaume mwenye vigezo hivyo, lakini pia anapaswa kujua kwamba
Lulu Diva ni...
msichana mrembo na anayependa sana kudekezwa.
“Mpaka mtu awe na mimi kwenye mahusiano
kuna vigezo naviangalia. Kwanza kabisa nampenda mwanaume smart mind, mtu
ambaye ameshika dini anamuheshimu Mungu, pia gentlemen kama hivyo awe
ananidekeza awe ananijali, , understanding, passion na Sacrifice,"
Msanii huyo ambaye ni zao la warembo
waliokuwa wakipamba nyimbo za wasanii kabla ya kugeukia tasnia ya
uimbaji amesema pamoja na kupenda kwake kudekezwa haimaanishi kwamba
anababaishwa na vitu vidogo vidogo, La! hasha yeye ni mrembo lakini pia
mtafutaji anayejituma.
0 comments:
Post a Comment