Tuesday, July 18, 2017
MADEE AWAJIBU WALIOSEMA ANAANDIKIWA NA RAYVANNY
Kitaani kulikuwa na tetesi kumuhusu mkali wa muziki kutoka Manzese Madee zikidai kwamba mkali huyo hivi sasa hafanyi poa kwenye game kutokana na kuwa alikuwa amezoea kuandikiwa ngoma na Rayvanny ambaye kwasasa yuko chini ya lebo ya WCB.
Leo Madee ameamua kuzitolea uvivu story hizo na kudai kwamba yeye yuko kwenye game kwa miaka 16 sasa ikiwa huyo Rayvanny ndio kwanza ana miaka 3.
Madee amedai ameanza kutengeneza hits tangu mwaka 2001 kipindi ambacho hata huyo Rayvanny hajajua muziki ataanza lini, inakuwa...
vipi leo hii isemekane kwamba yeye anamtegemea Rayvanny.
“Ray anayo nafasi ya kuniandikia kama mimi nitaamua, lakini sio mimi kumtegemea Ray kuniandikia ngoma. Kama hicho nakitaka nitakifanya kwasababu sio kwamba ni kosa na wala sioni tatizo, ila suala la mimi kuandikiwa ngoma zangu na Ray hivyo ni vity viwili tofauti.” Alisema Madee
Kwa msisitizo Madee amefunguka kuwa ameanza kuandika ngoma miaka 16 iliyopita na pia amekanusha vikali suala na kuwahi kuandikiwa ngoma na Rayvanny.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment