Rapa Young Killer Msodoki amedai mtandao wa kijamii wa Instagram
umesababisha wasanii wengi kuchukuliwa poa na mashabiki hasa wa hip hop
kwa kuwa wanachokipenda zaidi ni umbea kuliko kufuatilia kazi za msanii
mwenyewe anazozifanya katika muziki wake.
Young
Killer amebainisha hayo baada ya kuwepo dimbwi kubwa la mashabiki
kufuatilia na kuchimbua maisha binafsi ya wasanii na kuwaanika katika
mitandao mbalimbali ya kijamii jambo ambalo limepelekea watu kupenda
'udaku' zaidi kuliko...
hata kujua ni kazi gani mpya ya msanii ameitoa au
anaifanya kwa kipindi hiki.
"Now days watu wamekuwa
wanapenda vitu vya hovyo sana yaani vile vitu 'real' ambavyo vinafanya
sisi tuwe katika nafasi ambayo tulikuwepo vinakuwa vinapotezwa na vitu
vya 'kipumbavu' sana", amesema Youngkiller.
Pamoja na hayo, Young Killer ameendelea kwa kusema "mitandao
imekuwa mingi, maisha yetu yote sasa hivi watu wanatuchukulia poa tu,
so hiyo nadhani inachangia kushusha hata 'mode' ya kufanya kazi nzuri".
Msodoki pia amedai wasanii wengi wanao-rap bongo wanaogopana kuchana wenzao ndiyo maana 'game' imepoa.
0 comments:
Post a Comment