Msanii Nandy amedai kwa sasa yupo kwenye mazoezi makali ili kutengeneza mwili mzuri wenye muonekano na mvuto mbele za watu.
Mbele
kamera za eNewz ya EATV, Nandy amekiri hayo na kusema kuwa amekuwa
akipokea ushauri kwa watu mbalimbali wakimtaka atengeneze muonekano na
ndio ameanza...
mazoezi 'squat' kutengeneza tumbo pamoja na 'shape'.
"Nataka nitengeneze 'shape'
yangu iwe nzuri, niwe na muonekano wa mazoezi. Na kwa vile mimi ni mtu
wa kufanya show natakiwa niwe strong japo sina tumbo kubwa nataka niwe
na six pack lakini 'very sexy'. Mimi nina ndoto za kuwa msanii wa
kimataifa hivyo muonekano kwangu ni kitu cha muhimu isitokee siku
nakutana na Ciara akaanza kunishangaa. Mfano aseme huyu katokea wapi", Nandy alisema.
Nandy ameendelea kufunguka
"Sitegemei kufanya Surgery kujiongezea chochote kile, labda itokee siku
moja nikanenepa kwa vile sasa hivi miili haikubali kwani tunatafuta
maisha kwa nguvu zote. Ikitokea nimenenepa watu wasidhani nimefanya
upasuaji kwani unene na surgery vinatofautiana lakini mazoezi nayofanya
yatanitengenezea shape kidogo" aliongeza.
0 comments:
Post a Comment