
Msanii mkongwe wa bongo fleva, Lady Jay Dee maarufu kama 'Komando Jide" amefunguka na kudai haoni sababu ya yeye kutoa wimbo mpya kila mara kwa madai nyimbo zake ni za hisia ambazo zinaweza kuishi miaka mingi.
“Siwezi kutoa nyimbo mpya
kila siku, kwa sababu nyimbo zangu ni za hisia, ambazo zinaweza kuishi
hata miaka 10. Ni bora nitoe wimbo mmoja kwa mwaka lakini...
uwe unaishi miaka mingi kwa ladha ile ile siku zote," amesema Jay Dee.
uwe unaishi miaka mingi kwa ladha ile ile siku zote," amesema Jay Dee.
Pamoja na hayo, Jay Dee amesema wasanii
wengi wa kike wanashindwa kupambana katika muziki kutokana na kutopewa
ushirikiano wa kutosha katika kile wanachokifanya japokuwa muda mwingine
uongozi nao unachangia.
Lady Jay Dee ameachia ngoma ya 'I miss you' iliyotengenezwa na 'producer' Man water.
0 comments:
Post a Comment