Msanii wa bongo fleva, Linah Sanga amefunguka na kudai hakuwa
amejipanga kwa kipindi hiki kuwa na mtoto ila anamuomba Mungu isiwe
kigezo cha yeye kupotea katika muziki ili aje kuwa mfano kwa wasanii
wenzake wa kike wanaogopa kubebea ujauzito.
Linah
amebainisha hayo baada ya kuwepo imani kwa baadhi ya watu wakidai msanii akioa,
akiolewa hata akijifungua na mtoto mara nyingi hawezi...
kuendelea kufanya
vizuri katika kazi zake kwa kuwa majukumu ya ulezi yanaongezeka na
kupelekea kupotea katika 'industrial' ya muziki.
"Nina muomba Mungu usiku na
mchana nisije kupotea katika 'game' kwa sababu ya uzazi, ili iwe mfano
hata kwa wengine ambao watakuja nyuma yangu, labda wanaogopa kuzaa kwa
kufikiri watapotea. Ila mimi nafikiri ni jinsi mtu mwenyewe anavyoishi
na mashabiki zake", amesema Linah.
Pamoja na hayo, Linah ameendelea kwa kusema "Sikuwa
nimejipanga kupata mtoto katika kipindi hiki ila nilikuwa na-wish
nipate ujauzito nizae lakini sikufahamu ni lini itanitokea hivyo. 'So'
kipindi kile nilichokuwa na-wish nikawa kila nikijaribu haingii,
nikajisahau na kujikuta imekuja hata sikutarajia, lakini kwa kuwa
nilikuwa nina uhitaji nikasema hakuna neno. Japo nilishauriwa vitu vingi
sana mwanzoni lakini nikasema hapana kwa kuwa nimetaka kuzaa acha
nifanye hivyo", amesisitiza Linah.
0 comments:
Post a Comment