Pages

Subscribe:

Sunday, September 17, 2017

LADY JAYDEE: TANZANIA HAKUNA AMANI MTU KUPIGWA RISASI INATISHA

Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee amefunguka na kusema kwa hali ilivyo sasa Tanzania ni wazi kuwa amani haipo kama alivyokuwa kipindi cha nyuma na kudai hali hiyo inaleta hofu miongoni mwa wananchi. 

Lady Jaydee alisema hayo na kusema kitendo cha Mbunge Tundu Lissu pamoja na Meja Jenerali mstaafu wa JWTZ, Vincent Mritaba kupigwa risasi na watu wasiojulikana ni wazi kuwa...
amani ya nchi haipo. 

"Ni kweli Tanzania hakuna amani kwa sababu kitendo cha mtu kupigwa risasi hadharani inatishia amani ukizingatia kuna wasanii wengine walikuwa wanatekwa unaogopa, sehemu yenye amani vitu kama hivyo haviwezi kutokea, na kitendo cha Meja mstaafu wa JWTZ kupigwa naye risasi inaongeza kabisaa kuwa Tanzania amani haipo naweza kuwa sina la kusema ila nikaishia kusikitika tu" alisema Lady Jaydee 

Aidha Lady Jaydee anasema matukio haya yanaotoa picha mbaya kuwa kama nchi tunakokwenda si sehemu nzuri 

Mbali na hilo Lady Jaydee kwa sasa ameachia  wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'I miss you' uliotengenezwa na mtayarishaji Man Water kutoka Combination Soound.

0 comments:

Post a Comment