Msanii wa filamu nchini Ray Kigosi amefunguka na kumpa sifa mzazi
mwenzake Chuchu Hansy ambaye leo alikuwa anasherekea kumbukumbu ya siku
ya kuzaliwa kuwa bado ni mbichi licha ya kujifungua siku za karibuni.
ambavyo huenda alikuwa akidhani labda akipata mtoto anaweza kuharibika na kupoteza muonekano wake.
"Mzungu wangu bado mbichi
utafikiri ujajifungua juzi kweli kujifungua siyo kuzeeka 'Happy birthday
to you mama Jaden Chuchu Hans" aliandika Ray Kigosi.
"Asante sana kwa kuwa mama
bora kabisa kwa mwenetu Jaden hakika hakuna wa kufanana na wewe nina
mengi sana ya kukwambia ila wacha leo kwenye siku yako ya kuzaliwa
nikwambie haya machache nakupenda, nakuthamini na kukujali. Pia nitakuwa
nafanya kosa kubwa kama sitomshukuru Mungu kwa kunizalia mtoto mzuri na
kunipa heshima kubwa ya kuitwa baba" aliandika Ray Kigosi
0 comments:
Post a Comment