Nyota wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo usiku wa jana
amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa kiume duniani akimubwaga
mpinzani wake Lionel Messi wa Barcelona.
Katika
tuzo hizo zilizofanyika jijini London Ronaldo ametwaa tuzo hiyo ambayo
sasa inamfanya kuhama kundi la Lionel Messi na kuingia kwenye kundi la
Ronaldo De Lima na Zinedine Zidane ambao...
wametwaa tuzo hiyo mara tatu
kila mmoja.
Ronaldo ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya
pili mfululizo na kufikisha idadi ya tuzo tatu ambapo mara ya kwanza
alitwaa mwaka 2008 akiwa Manchester United.
Mwaka 2009 FIFA iliungana na chama cha
soka cha Ufaransa na kuunganisha tuzo hiyo ikafahamika kama Ballon d.or
ambapo Messi aliitwaa kwa mara ya kwanza. Mwaka 2016 FIFA walivunja
mkataba wao na Ballon d’or kisha kurejesha tuzo ya FIFA ambapo Ronaldo
alitwaa pamoja na mwaka huu.
Naye Kocha wa Real Madrid Zinedine
Zidane amekuwa kocha bora wa soka la wanaume (BEST FIFA MEN’S COACH
2017) akiwagalagaza Massimiliano Allegri wa Juventus na Antonio Conte wa
Chelsea.
0 comments:
Post a Comment