Mara kadhaa nikki amekuwa akipost point ktk mitandao yake ya kijamii ambazo kwa mtu mwelewa akisoma na kutafakari hawezi kutoka patupu lazma ujengeke kwa kiasi fulani na sasa Nikki ameamua kuweka wazi mambo makuu 8 atakayo yafanya endapo atakuwa Rais hapo baadae. Nitakapo kuwa Rais hapo baadaee inshalla
1. Kikaoo kikubwa cha serikali yangu sio baraza la mawaziri itakuwa...
mkutano mkuu wa kijiji/ mtaaa (kitaa kinaongea)
2. Kipimo cha maendeleo kitakuwa kupanda au kushuka kwa maisha ya watu sio vipimo vya kukua kwa uchumi, makusanyo, au shilingi.. .
3. Mfumo wa elimu utajikita kupima "learning" yani kujifunza sio kupima ufaulu na ufeli
4. Vyama vyenye nguvu vitakavyo kuwa vina fanya mikutano na kuihoji serikali sio vyama vya siasa bali vyama vya wakulima, wafanyakazi, walimu, machinga, boda boda, madactari nk
5. Serikali itakuwa mdau namba moja kwenye uchumi na mwekezaji atakuwa mkulima, mfugaji, mchimbaji mdogo, wavuvi wadogo na wafanyabiashara wa wadogo
6. Ardhi, elimu, maji, afya havitakuwa bidhaa bali hifadhi ya jamii
7. Maisha bila maadili hayana mana kila mtoto lazima afundishwe kuwa na adabu, uaminifu, heshima, ujamii, upendo, bidiii na kujiamini
8. Mahusiano na mataifa ya Afrika, hakutakuwa na neno wahamiaji haramu, mwafrika hawezi kuwa haramu afrika ni nyumbani kwao
Maswali mtaniuliza wakati wa kampeni ukifika....(mgombea binafsi)
0 comments:
Post a Comment