Mwanamitindo na Mfanyabiashara kutoka Kenya, Huddah Monroe, amefunguka
na kusema kwamba anadhanii Msanii Juma Jux wa Tanzania ni mwanaume
ambaye yeye anaweza kuwa naye kimahusiano huku akimmwagia sifa kuwa
anamuonekano mzurii kwenye mavazi.
Akifanya
mahojiano maalumu na kipindi cha Nirvana kinachorusha kila Jumanne saa
tatu usiku chini ya Mtangazaji Deogratius Kithama, Huddah alijibu swali
la mtangazaji huyo kama anaweza kuwa kwenye mahusiano na Jux baada ya...
kumsifia kuwa ana muonekano wa tofauti na wenye kuvutia.
"Aaah, Nafikiri ni mwanaume ambaye naweza kuwa naye kwenye mahusiano...... Yupo 'single? hata mimi nitapatikana....." amesema Huddah.
Aidha Huddah amemshauri Jux kufanya
kolabo na wasanii wakubwa zaidi wa kimataifa ili azidi kuwa msanii kubwa
zaidi ndani na nje ya kimataifa kwani anamuonekano wa kuwa mtu maarufu.
Mbali na hayo Huddah amekiri kwamba
alishawahi kumcheki Jux kupitia mtandao na kumwambia jinsi gani anapenda
muonekano wake wa mavazi na jinsi ambavyo anavaa tofauti na jinsi jamii
zinavyomfikiria.
0 comments:
Post a Comment