Pages

Subscribe:

Sunday, October 22, 2017

LINAH ASAFISHWA NA MUME WAKE JUU YA KASHFA HII

Mzazi mwenzake na Msanii wa bongofleva, Linah Sanga, amekanusha madai ya mpenzi wake huyo kumbana kiasi cha kukosa fursa ya kumuhudumia mwanae aliyempata na mwanamke mwingine na kusema "Linah ni mwanamke mwenye kipaumbele kwa mwanae kuliko alihisi. 

Akifunguka EATV kwenye kipindi cha Friday Night Live, Shaban Mchovu (mwanaume aliyezaa na Linah) amesema kwamba pamoja na umaarufu alionao...
mzazi mwenzake hajawi kuvimba au kupotezea suala la yeye kumuhudumia mtoto wake na amemsifu kwamba mara zote amekuwa akimkumbussha na kumsisitiza kufanya hivyo na sivyo kama maneno ya watu wengine yanavyosema.

"Linah ni mwanamke ambaye anachukulia vitu serious na siyo poa kama watu wanavyomuona kwa nje. Anachukulia kipaumbele sana kwa mwanangu, sijui kama anafanya hivyo nione kama anajali sana lakini wakati mwingine unaona ana moyo haswa wa kufanya hivyo. Sijutii kuwa na Linah na enjoy sana"

Akizungumza kuhusu Linah kuvunja mahusiano na mama mtoto wake wa kwanza ambaye tayari alishamvalisha pete ya uchumba, Bw. Mchomvu amekanusha na kusema kwamba Linah hakuhusika na kuvunja mahusiano yake bali ni yeye na mpenzi wake wa awali walishindwa kutatua matatizo yao.

"Chenye mwanzo huwa na mwisho. Matatizo yalitokea tukashindwa kuyatatua sisi wenyewe mwisho wa siku ikawa ni kama mkataba umeharibika. Na kuhusu kwamba uhusiano na mpenzi wangu huyo wa zamani ulisababisha afya yake kuzorota kama jinsi watu wanavyosema mimi sina taarifa hizo nachojua yupo vizuri na mimi na familia yangu mpya tupo safi"

0 comments:

Post a Comment