Tuesday, October 17, 2017
BELLA: SIYO CONGO TU HATA DUNIA NZIMA KUNA MABLACK WANA BOOST RANGI
Msanii wa muziki Bongo, Christina Bella amefunguka taarifa za kuwahi kujichubua. Muimbaji huyo ambaye asili yake ni nchini Congo amesema si kweli wasanii kutoka nchi hiyo wamekuwa na tabia ya kujichubua kama inavyokuwa ikienezwa bali ni tabia ya mtu binafasi.
“Ukisema niongelee watu mimi sijui, hata wabongo wanajichubua, hata wanigeria, dunia nzima kuna mablack wengine...
wanaboost rangi” Bella ameiambaia Bongo5.
“Unaniuliza kuhusu wale watu wa Congo siwezi kuongelea na siyo Wacongo wote wanajichubua, katika nchi yoyote kuna baadhi ya watu wanatabia fulani, kuna nchi nyingine wahuni wapo wengi lakini siyo wote wapo hivyo” ameongeza.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment