Msanii wa muziki wa injili Tanzania ambaye amejitengenezea mashabiki
wengi nchini Kenya, Christina Shusho, amesema kitendo cha yeye kutukanwa
na Wakenya kwa kumuombea Uhuru Kenyatta kilimuumiza lakini hakuwa na
nia mbaya.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Christina Shusho amesema kitendo hicho kwake kilimshtua lakini ni kawaida kutokana na mihemko waliyonayo wakenya sasa hivi, na hakufanya vile kwa...
nia mbaya au kuonyesha yuko upande gani.
Shusho ameendelea kusema kwamba kutokana na hilo alilazimika pia kumposti Raila Odinga ili aweze kuweka usawa, na kuwaombea Wakenya wote wafanye uchaguzi kwa amani.
“Unajua ile ni mihemeko tu inavyokuwaga kipindi kama hiki ambacho Wakenya wanapitia sasa , mimi nilikuwa nafanya maombi nikasema nimuombee na Rais wa Kenya, basi wakanijia juu, nikaanza tukanwa, wakatafutwa mpaka marafiki zangu wa kule nao wakawa wanatukanwa, ni kitendo ambacho kilinishtua, nikaona basi acha nimpost na huyu mwengine (Odinga) ili niweke usawa, lakini naomba watu wa Kenya watambue sikuwa na nia ya upendeleo au kuwagawa”, amesema Christina Shusho.
Hapo leo Oktoba 26, taifa la Kenya linaendelea kufanya uchaguzi wa marudio kama ambavyo iliamriwa na Mahakama ya Juu, baada ya kufuta matokeo ya Urais kwenye uchaguzi wa awali wa Agosti 8.

0 comments:
Post a Comment