Thursday, October 19, 2017
MSAMI: NANDY NI MDOGO WANGU SIJAWAHI KUTOKA NAYE
Msanii wa Bongo Flava, Msamii amesema si kweli kwamba ameshawahi kutoka kimapenzi na Nandy. Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma katika mahojiano na Bongo5 amesema Nandy ni kama dada yake hivyo hawezi kufanya hivyo.
“Nandy sijawahi kupita naye ni kama mdogo wangu, dada yangu, kwa hiyo kwa sasa hivi mimi na Nandy ni...
kaka na dada, let say mimi ni mtu ambaye nimetoka kwenye familia ya THT Nandy pia kwenye familia hiyo hiyo, tupo familia moja” amesema Msami.
Msami anaungana na rapper Bill Nass ambaye amekuwa akidaiwa kuwa na mahusiano na Nandy kitu ambacho amekuwa akikikanusha kila mara.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment