Pages

Subscribe:

Saturday, October 21, 2017

TWAWEZA WAKEKA WAZI ASILIMIZA YA WATANZANIA WANAOHITAJI KATIBA MPYA

Wawili kati ya Watanzania watatu wanadhani kwamba ni wakati taifa hilo linafaa kuwa na katiba mpya, kulingana na matokeo ya utafiti uliofanywa na Twaweza, Utafiti huo kwa jina ”Unfinished Business” unaangazia mkwamo wa mkakati wa katiba mpya kutokana na data ya sauti za wananchi.
 
Matokeo hayo yanatokana na data iliokusanywa kutoka kwa raia 1,745 nchini Tanzania bara kati ya...
mwezi Juni na Julai.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba nusu ya waliohojiwa ama asilimia 56 wanafikiria kwamba rasimu ya mwisho ya katiba inafaa kupigiwa kura ya maoni.

Hatahivyo utafiti huo unaonyesha kuwa nusu ya raia ambayo ni asilimia 48 wanaamini kwamba mkakati wa kuandika katiba mpya hautafanyika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Raia wanataka katiba itakayosisitiza uwajibikaji.

Watu wanane kati ya kumi wanataka nyadhfa za mawaziri kuthibitishwa na bunge ambayo ni asilimia 79 huku watu sita kati ya kumi wakitaka kupewa uwezo wa kuwaondoa wabunge katikati ya uchaguzi.

Afisa mkuu wa Twaweza Aidan Eyakuze alisema kuwa raia wanataka katiba mpya.
Wengi wanataka kuwepo kwa tume mpya ili kuwa na mwanzo mpya.

Lakini wengine wako tayari kuendelea na rasimu ya awali kutoka kwa tume iliopita, alisema.

Kulingana na utafiti huo, raia wamegawanyika katika hatua nyengine za uwajibikaji kama vile kuzuia akaunti za kigeni miongoni mwa viongozi na wanaharakati kama miongoni mwa maadili ya kitaifa.

0 comments:

Post a Comment