Pages

Subscribe:

Friday, October 27, 2017

MAUMBO YA WAKIMBIZI YAVUNJA NDOA ZA WATU KIGOMA



Maumbo ya wanawake wakimbizi kutoka nchi jirani ya Burundi huko mkoani Kigoma yamezua gumzo baada ya akina Baba kuzitelekeza familia zao na kuoa wanawake hao wakirundi. Baadhi ya Wanaume katika wilaya ya Kakonko wanadaiwa kutelekeza ndoa zao na kwenda kuoa wanawake hao wa Kirundi huku sababu ikiwa ni uzuri maumbo yao.

Hayo yameelezwa na wanawake wa kijiji cha Kaziramihunda, kilichopo kata ya Kasanda wilayani Kakonko mkoani Kigoma mbele ya Mkuu wa...
wilaya hiyo, Kanali Hosea Ndagala.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wa kijiji hicho Bi. Tabu Kiuliko amesema anamuomba Mkuu wa Wilaya kuingilia kati suala hilo la kutelekezwa na wanaume zao kwani limekuwa sugu na limerudisha nyuma maendeleo ya baadhi ya familia.

“Wanawake wengi wameachiwa jukumu la ulezi wa familia baada ya waume zao kuwatelekeza wake zao na kuoa wakimbizi , tunaomba serikali iingilie kati suala hilo,“amesema Bi. Tabu.

Hata hivyo, Afisa Mtendaji wa kata ya Kasanda, Motoni Borutu ameunga mkono taarifa hiyo kwa kukiri kuwa Ofisi yake imepokea malalamiko hayo na kuahidi kuyafanyia kazi.

Kwa upande mwingine, Afisa Uhamiaji wa wilaya ya Kakonko, Christopher Mlemeta ambaye alikuwa kwenye msafara huo wa mkuu wa wilaya, amesema ni kosa kisheria kwa mtu kuoa au kuolewa na mkimbizi na kuishi naye nchini bila kupata kibali maalumu kutoka serikalini.

0 comments:

Post a Comment