Kesi inayomkabili Muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu', imeendelea leo
katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo ushahidi wa upande wa
utetezi uliokuwa ukisubiriwa umewasilishwa na kusomwa na Polisi
Detective Sergeant Nengea aliyerekodi ushahidi huo kutoka kwa aliyekuwa Daktari wa Marehemu Steven Kanumba.
Katika ushahidi uliosomwa na Sergeant
Nengea (ambaye mahakama imemtambua kama shahidi) ambao aliurekodi kutoka
kwa Josephine Mushumbusi umedai kwamba...
"Marehemu alikua na matatizo ya
damu, upungufu wa hewa kwenye ubongo, alikuwa anasikia maumivu katika
ubongo na akili kuchoka".
Aidha ushahidi huo umekamilisha kesi
hiyo siku ya leo lakini Wakili Kibatala ameiomba mahakama kumruhusu
kumpatia nafasi ya kutoa hoja za ziada ambazo zitasaidia katika kufanya
maamuzi juu ya kesi hiyo.
Hata hivyo Jaji Sam Rumanyika amesema
kesho wazee wa baraza watakaa na kujadili kama Lulu ana hatia katika
kesi hiyo inayomkabili au hana, na kusubiria kupanga siku ya hukumu.
0 comments:
Post a Comment