Thursday, October 26, 2017
MWILI WA MFALME WA THAILAND KUCHOMWA MOTO SIKU YA LEO
Waombolezaji kote Thailand wanafanya matembezi kunaadhimisha sehemu kuu ya siku tano za sherehe za mazishi kwa ajili the Mfalme Bhumibol Adulyadej aliyeaga dunia.
Mfalme huyo alifariki Oktoba 2016 akiwa na umri wa miaka 88.
Mwili wake utateketezwa kwa moto baadaye Alhamisi, Kwa taratibu za kifalme zitakazoongozwa na...
mwanae na mrithi wake, Mfalme Maha Vajiralongkorn.
Taratibu za mazishi zilianza Jumatano kwa sherehe za kubudha ,kwenye kasri Kuu la kifalme.
Leo Alhamisi imetangazwa kuwa siku ya mapumziko, ambapo biashara nyingi zitafungwa kwa siku ama kwa nusu siku.
Mapema Alhamisi, mwili wa mfalme huyo utaletwa kwenye eneo maalum utakapochomwa kutoka kwenye Ukumbi wa Kifalme ulipo katika Kasri kuu kwa ajili ya kuteketezwa.
Wajumbe wa familia ya ufalme wa Thailand na waheshimiwa kutoka nchi 40 watahudhuria mazishi hayo ya kuchomwa kwa mwili wa hayati mfalme Bhumibol Adulyadej , huku umati mkubwa wa watu ukitarajiwa kujipanga kwenye mitaa ya karibu.
Majivu ya Mfalme hatimae yatakusanywa na kusafirishwa hadi kwenye kasri la Ufalme Ijumaa.
Sherehe zitaendelea kwa siku mbili Zaidi.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment